Untitled Document
home | tume | utangazaaji | znz

Ijue Treni ya Zanzibar

Na Dkt Juma Mohammed, MAELEZO Zanzibar

Ni miaka 97 tangu huduma za usafiri na usafirishaji kwa kutumia Treni ziliposimama rasmi Visiwani Zanzibar. Vijana wengi wa leo pengine hii itakuwa ni habari mpya kwao, lakini iliyokongwe kwa wazee waliowengi.

Historia ya usafiri wa treni kamwe haiwezi kuzungumzia maendeleo ya usafiri huo bila kuitaja Zanzibar. Treni ya Zanzibar ilianza mapema zaidi kuzipita nchi zote za Afrika Mashariki na pengine hata baadhi ya nchi za Ulaya ya kale.

Usafiri wa treni ulianza Zanzibar mwaka 1888 treni iliyokuwa ikivutwa kwa Punda, lakini mageuzi ya viwanda huko Ulaya na ukuaji wa teknolojia ulibadili mfumo mzima wa miundombinu ya treni.



Ilikuwa Mwaka 1904 Zanzibar ilisaini mkataba wa ujenzi wa reli ya kisasa na kampuni ya Kimarekani ya “Arnold Cheney and Co” kujenga reli iliyoanzia Bububu nje ya Jiji la Zanzibar hadi Ngome Kongwe.

Safari ya kwanza ya abiria ilianza mwaka 1905 kwa treni ya steam kwa umbali wa maili saba kutoka kwenye kasri la Sultani mjini Zanzibar, ilipita katika upwa wa Magharibi hadi Kijiji cha kando kando ya bahari cha Bububu.

Miundombinu ya barabara iliyopo hivi leo, haikuwepo katika zama hizo, Serikali ya kikoloni haikujihusisha sana na ujenzi w miundombinu ya barabara.

Kwa sehemu kubwa treni ya Bububu ilitegemewa sana na wakati wa nje ya mji kuja mjini. Kwa wale ambao walitaka kuona mandhari ya visiwa waliweza kutumia behewa la sehemu ya kwanza.

Mbali ya kusafirisha abiri na mizigo, reli hii ilitumika katika kusambaza teknolojia ya umeme katika visiwa hivi. Wakati wa ujenzi wake, kampuni Arnold Cheney and Co” ya Marekani ilikuwa na kazi ya kuweka waya za umeme pembezoni mwa reli hiyo.

Treni ya Bububu imesita kufanyakazi mwaka 1930.

MWISHO..

Habari zaidi za Zanzibar