Untitled Document
home | tume | utangazaaji | znz

Samatta aendelea na unahodha KRC GENK

SAMATTA AENDELEA NA UNAHODHA KRC GENK IKIENDELEZA WIMBI LA USHINDI LIGI YA UBELGIJI

Na Mwandishi Wetu, GENK
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta kwa mara nyingine tena jana alikuwa Nahodha wa klabu yake, KRC Genk ikiibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Royal Excel Mouscron katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk.
Katika mchezo wa jana, mabao ya Genk yote yalifungwa na mshambuliaji mpya, Mnigeria Ebere Paul Onuachu aliyesajiliwa kutoka Midtjylland ya Denmark dakika ya 75 na 90 na ushei, wakati la Royal Excel Mouscron lilifungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Ghana, Jonah Osabutey dakika ya 49.
Sasa KRC Genk imefikisha 16 baada ya kucheza mechi tisa, ingawa inaendelea kukamata nafasi ya sita, ikizidiwa pointi saba na vinara, Club Brugge wanaofuatiwa na Standard Liege yenye pointi 20 za mechi 10, Gent pointi 17 za mechi tisa sawa na Antwerp na Mechelen ambayo imecheza mechi 10..

Habari zaidi za Michezo