Untitled Document
home | tume | utangazaaji | znz

Safari za ndege zaanza uwanja wa ndege wa kimataifa

Polisi wakilinda ukumbi wa kuondoka abiria wa uwanja wa ndege wa Hong Kong baada ya waandamanaji kupambana na polisi jana yake, Agosti 14, 2019. REUTERS/Thomas Peter - RC1392D57540.

Safari za ndege zimeanza Jumatano baada ya jaji wa mahakama mmoja kutoa amri ya muda kudhibiti maandamano ya kupinga serikali yaliyo sababisha shughuli za usafiri kusitishwa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa, Hong Kong.

Mamlaka ya viwanja vya ndege ya Hong Kong imetangaza Jumatano kuwa jaji ametoa amri ya muda ya kudhibiti maandamano ya kuipinga serikali, katika moja ya uwanja wa ndege mkubwa duniani, ambapo kwa siku mbili waandamanaji walikuwa wameleta ghasia kwa kupambana na polisi.

Amri hiyo inawataka waandamanaji kuwepo katika maeneo maalumu, ikiwa ni juhudi za kuzuia msongamano ambao ulisababisha wafanyakazi wa serikali na mashirika ya ndege kurudishwa majumbani ikiwa pamoja na kusitisha safari zote za ndege za kutoka na kuingia katika himaya hiyo ya China.

Hatua hiyo ilisababisha wasafiri wa ndege kutojua la kufanya na kutokuwa na uhakika wa lini wata-endelea na safari zao huku wakishindwa kununua chakula na kukokosa mahala pa kulala..

Dunia yetu