Untitled Document
home | tume | utangazaaji | znz

Mdororo wa uchumi duniani na migogoro ya kimataifa kugubika mkutano wa G7 Biarritz



Nchi za zilizostawi kiuchumi duniani (G7) zinakutana katika mji wa Biarritz kusini magharibi mwa Ufaransa kuanzia Agosti 24 hadi 26, wakati uchumi wa dunia unaendelea kushuka na machafuko mengi, hasa barani Asia, vinaendelea kuzua mvutano wa kimataifa.

Ukuaji wa chini, kushindwa kulipa madeni mbalimbali, kuzorota kwa zoezi la kutoa mikopo, gawio la chini ...vyote hivyo vinatarajiwa kuzungumziwa katika mkutano wa nchi ziliostawi kiuchumi duniani (G7). Uchumi wa Uingereza na Ujerumani, mabingwa wa Ulaya kwa uchumi wa kiwango cha juu, ulianza kupanda katika msimu wa pili wa mwaka.

China, uchumi wake umepungua kwa kiasi kikubwa, kutokana na kwamba shughuli ya uingizaji bidhaa nchini imekuwa dhaifu. Nchini Marekani, kiwango cha uzalishaji kimeshuka mara mbili mwezi huu. Yote hayo ni dalili zinazoonyesha kuwa uchumi duniani umeshuka.

Mvutano wa kibiashara kati ya China na Marekani, lakini pia kati ya Ulaya na Marekani umeongeza dosari katika kushuka kwa uchumi duniani na hivo kuweka mashaka mengi kuhusu mauzo ya nje, na pia nia ya Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya.

Lakini viongozi wa kisiasa kutoka nchi zilizostawi kiuchumi (G7) na wamiliki wa makampuni makubwa kutoka nchi hizo wanaweza kwenda mbali zaidi ya yale waliyokuwa wamekubali kuunga mkono uchumi: Tume ya Ulaya haijawahi kuwa makini kuhusu nakisi ya bajeti na viwango vya riba bado ni vya kiwango cha chini kabisa, miaka kumi baada ya mdororo wa ya fedha na kiuchumi..

Dunia yetu