Untitled Document
home | tume | utangazaaji | znz

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar

Zanzibar ni Nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote laVisiwa vya Unguja na Pemba pamoja na Visiwa vidogo vilivyoizungukana bahari yake ambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika naZanzibar ikiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.

Zanzibar ni miongoni mwa Nchi mbili zinazounda Jamhuri yaMuungano wa Tanzania.

Kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za Serikali, Raisaweza kuigawa Zanzibar katika Mikoa, Wilaya na maeneo mengineyokwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria iliyotungwa na Baraza laWawakilishi.

Zanzibar itafuata mfumo wa Kidemokrasia wa Vyama Vingi vya Siasa wenye kuheshimu utawala wa sheria, haki za binaadamu,usawa, amani, haki na uadilifu.

Zanzibar itafuata mfumo wa mgawanyo wa madaraka katiya mamlaka tatu, Mamlaka ya Utendaji, Mamlaka ya Kutunga Sheriana Kusimamia Utekelezaji wa Shughuli za Umma na Mamlaka yaKutekeleza Utoaji Haki.

Mamlaka ya Utendaji ni Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,Mamlaka ya kutunga Sheria na Kusimamia Utekelezaji wa Shughuliza Umma ni Baraza la Wawakilishi na Mamlaka ya Kutekeleza Utoaji Haki ni Mahkama..

Habari zaidi za Zanzibar