Untitled Document
home | tume | utangazaaji | znz

Hadithi za Chukwani



Asili ya Chukwani

Imesimuliwa na Mzee Suleiman Khamis Faraji


Hapo zamani katika kijiji hiki waliishi watu, sio wengi sana kwani nyumba zilihesabika. Miongoni mwa watu hao alikuwepo bibi na wajukuu zake ambao aliwapenda sana na aliwapa kila walichotaka amba-cho aliweza kukimiliki.

Kwa bahati mbaya kijiji hiki kilikuwa hakina jina.Siku moja wale watoto walikiona kitu ndani ya nyumba yao.

Kile kitu yule bibi alikihitaji na wale wali-kipenda sana kile kitu kiwe chao.

Kwa hivyo walimshika sana bibi yao awape kile kitu kwa kusema, bibi tupe we, bibi tupe. Yule bibi aliwanasihi wale watoto wawe na subira kwani subira huvuta heri.

Lakini wale watoto kwa pupa za kukitaka kile kitu waliendelea kumshikilia bibi yao awape kile kitu mpa-ka akakasirika na kuhamaki sana. Kwa ukali yule bibi aliwambia wale wajukuu zake maneno yafuatayo:- Chukwani kwa maana ya kuwa wachukue – kile walichokuwa wanakihitaji.

Kwa bahati nzuri walipita watu karibu na ile nyumba nakusikia yale maneno anayozungumza yule bibi na wajukuu zake kwa hasira pamoja na yale maneno aliyoyasema „Chukwani“.

Kwa hivyo walipokuwa wakipita karibu na ile nyumba ya yule bibi husema; „Bibi Chukuwani leo yupo?“ Nao humsalimia na kwenda na safari zao.

Ile hali ikaendelea kwa muda mrefu mpaka yule bibi alipofariki. Ile sehemu watu wakaipa jina kutoka lile neno chukuwani na kuliita eneo hilo „Chukwani.“ Ndio maana hadi sasa eneo hilo linaitwa kijiji cha Chukwani

Mwisho.


Makala haya kwa hisani ya

Soma na uwasomeshe wengine

Ni mradi wa Jumuiya ya Kijerumani (RAA) iliyopo wilayani Brandenburg, Ujerumani.

Habari zaidi za Zanzibar