Untitled Document
home | tume | utangazaaji | znz

Mafanikio Sekta ya Elimu Zanzibar

Na Dkt Juma Mohammed, MAELEZO

Ni jambo lisilokuwa na ubishi kuwa elimu ndicho chanzo muhimu kabisa kitakachomletea maendeleo na ukombozi wa kweli, elimu inawatoa wanadamu katika gugu la ujinga.

Umuhimu wa elimu umelezwa kwa kina katika vitabu vya dini, lakini pia mafundisho ya wanafalsafa wengi wamejikita katika kuhimiza watu kusoma kujiongezea maarifa katika fani mbalimbali.

Marehemu Nelson Mandela aliwahi kusema kwamba “Elimu ni silaha madhubuti inayiwoza kubadili dunia” Umuhimu wa elimu namna ulivyosisitizwa na wanafalsafa wengi hauwezi kupimwa katika kipimo chochote kile.

Ulimwengu wa leo unavyozidi kusonga mbele kwa wavumbuzi kutumia vipawa vyao, elimu itamsaidia sana mwanadamu kutokuachwa nyuma katika masuala mbalimbali yanayoendelea katika jamii.

Katika dunia inayoungana kimawasiliano na kugeuka kuwa kijisehemu kidogo, elimu inakuwa nguzo, hazina na daraja litakalomvusha binadamu katika hali yake ya unyoge wa fikra, mawazo na atayatanua maisha yake kuendana na maendeleo endelevu.

Ni miaka tisa sasa tangu Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt Ali Mohamed Shein alipoingia madarakani, wananchi wana kushuhudia mabadiliko makubwa katika sekta ya elimu.

Ukiondoa Rais wa kwanza wa Zanzibar, Mzee Abeid Amani Karume, Rais Dkt Shein anatajwa kuwa Kiongozi aliyeweka rekodi kubwa zaidi ya uwajibikaji kwa kugeuza Zanzibar kutoka katika mawazo mgando na kuanza kuijenga nchi huku akiamini kuwa Umoja na Amani ndio silaha madhubuti ya kufikia malengo mbalimbali.

Kama kuna jambo ambalo Zanzibar na Rais Dkt Shein anaweza kujivunia ni kuvuka malengo ya Millenia kupitia mpango wa elimu kwa wote ambapo Mataifa yanayoendelea yametakiwa chini ya mpango huo kutoa elimu kwa wote hadi ifikapo mwaka 2015.

Wakati hata kabla ya nusu ya muda uliowekwa, tayari Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeshakamilisha maazimio na malengo ya Milenia kwa kiwango cha juu kabisa kuliko nchi nyengine ambazo nyingi zinasuasua.

Sekta ya elimu imeonesha mafanikio makubwa na zaidi pale mkakati wa Serikali kuongeza idadi ya Skuli za Sekondari ulivyosimamiwa kwa umakini utekelezaji wake.

Zanzibar imeweza kutekeleza malengo ya millennia kuhusu elimu, Idadi ya skuli zimeongezeka ambapo Skuli za maandalizi sasa zimefikia 270 kutoka 238 mwaka 2010.

Takwimu za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar zinaonesha kuwa Skuli za msingi zimeongezeka kutoka 299 mwaka 2010 hadi Skuli 370 mwaka 2016 ambapo Serikali imekamilisha ujenzi wa skuli mpya 10 za ghorofa ili kuongeza nafasi kwa wanafunzi.

Hivi karibuni Rais Dk. Shein alisema kwamba Ili kwenda sambamba na mabadiliko ya sayansi na teknolojia, Serikali inatekeleza mradi inaohusiana na masomo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika skuli za msingi 248.

Skuli hizo zimepatiwa vifaa mbali mbali ikiwa ni pamoja na Kompyuta, Vitabu na vifaa vyengine vya ufundi wa TEHAMA pamoja na kuwapatia mafunzo watendaji wanaosimamia mradi huo.

Uongozi wa Rais Shein pia umetilia mkazo suala zima la kuimarisha mazingira ya ufundishaji na usomaji ambapo walimu wamekuwa wakiendelea kupatiwa mafunzo mbalimbali ya kuwaongezea ujuzi.

Wanafunzi nao wameendelea kujengewa mazingira bora zaidi ya kujifunzia ikiwa pamoja na kujenga Skuli mpya 21 ili kuongeza nafasi, huku SMZ ikizifanyia matengenezo makubwa skuli sita za sekondari Unguja na Pemba na kuzipatia vitabu na vifaa vya maabara pamoja na samani.

Mwenye macho haambiwi tazama, katika kipindi cha miaka tisa ya uongozi wa Rais Dkt Shein, Serikali imeweza kujenga Skuli mpya za Sekondari 19 Unguja na Pemba. Skuli 19 zilizojengwa ni za kisasa na tena ni miongoni mwa Skuli za mfano miongoni mwa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Skuli hizi 19 na 10 zilizokamilika kujengwa hivi karibuni ni mkombozi maana lile tatizo lililokuwa likiwakabili watoto kutembea masafa marefu au kusoma katika Skuli zisizokuwa na nafasi ya kutosha sasa limemalizika.

Aidha, tunaweza kuona pia Serikali imechukua jitihada maalum katika kuhakikisha watoto wenye mahitaji maalum wanapata haki yao ya elimu katika skuli mbali mbali, kupitia mpango wa elimu mjumuisho.

Uamuzi mwengine uliofanywa na Serikali ni kuyaimarisha mafunzo ya elimu ya amali na ufundi katika vituo vya Mwanakwerekwe, Mkokotoni na Vitongoji.

Vituo hivyo vimetoa mchango mkubwa wa kuwapatia vijana mafunzo mbali mbali ya fani za ufundi zikiwemo uashi, useremala, ushoni, uhunzi, upishi, uchoraji, ufundi bomba, ufundi umeme, magari, mafriji, teknolojia ya habari na fani nyenginezo.

Kama kuna jambo ambalo Zanzibar na Rais Dk. Shein anaweza kujivunia ni kuvuka malengo ya Millenia kupitia mpango wa elimu kwa wote ambapo Mataifa yanayoendelea yalitakiwa chini ya mpango huo kutoa elimu kwa wote mwaka 2015.

Wakati hata kabla ya nusu ya muda uliowekwa ulikuwa bado haujamalizika, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar tayari ilikuwa imeshakamilisha maadhimio hayo ya Umoja wa Mataifa na malengo ya Milenia kwa kiwango cha juu kabisa kuliko nchi nyengine ambazo nyin.

Habari zaidi za Zanzibar