Untitled Document
home | tume | utangazaaji | znz

Mtu kwao ndio Ngao

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Viongozi mbali mbali na wanadiaspora katika Kongamano la Tano la Diaspora Tanzania lililofanyika katik

Na Dkt Juma Mohammed, MAELEZO Zanzibar

Watanzania na hasa wale manazi wa muziki wa dansi bado wanaikumbuka ile band maarufu iliyowahi kutamba siku hizo ya Orchestre Safari Sound (OSS) iliyokuwa ikitumia mtindo wa Ndekule. Moja ya kibao chake ni “Usimchezee Chatu”.

Usimchezee chatu ohoo! chatu ehee! Dongo usimtupie, utaukosa ushindi!.

Natoa onyo kwa yeyote anayechezea chatu ni hatari,Atakuwa asipate lolote la manufaa Na ajali imkute bila ya kutegemea!

Atakuja adhirika ajute na Dunia.

Nami sitaki kumchezea chatu maana ninaweza kuadhirika,kujuta na dunia.Kwa kuchelea hayo nitaungana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Issa Haji Ussi Gavu katika ujumbe wake alioutoa kwa Wanadiaspora waliokutana hapa Zanzibar katika kongamano lao Diaspora.

Waziri Gavu ameweka bayana msimamo wa Serikali katika kuweka mazingira rafiki na yasiyokuwa yenye vikwazo kwa Watanzania wanaoishi nje ya nchi kutofanya ajizi na badala yake wawekeze nyumbani katika sekta mbalimbali ikiwa ni akiba yao ya sasa, kesho na hata hapo baadae.

Naungana nae kwa sababu sitaki kuukosa ushindi, sitaki kugeuka ngoswe penzi kitovu cha uzembe kama alivyoandika mwandishi Ewdin Semzeba katika riwaya yake inayovutia wasomaji wengi.

Kwa mnasaba huo nitaanza kwa kuchambuwa suala zima alilosema Waziri Issa Gavu la wanadiaspora wa Kitanzania kujipanga kuwekeza hapa nyumbani wito ambao unaakisi kauli mbiu ya kongamano la tatu la Diaspora “Mtukwao ndiongao”.

Naam! Mtu kwaondio ngao maana nyumbani ni nyumbani tu. Kwa kutambua ukweli huo, Waziri Issa Gavu ametoa mwanga kwa Wanadiaspora kuzitumia fursa za ufunguaji milango katika kuwekeza miradi mikubwa na midogo huku Serikali kwa upande wake(SMZ) ikiwa katika hatua za mwisho za kuwasilisha sera ya Diaspora na hapo baadae kuwa na sheria juu ya jambo hilo.

Kongamano la mwaka huu limefanikiwa kwa sehemu kubwa sio tu kwa wanadiaspora kuja kwa wingi, lakini pia umakini wa Serikali katika kufanikisha malengo na mikakati mbalimbali kuhusu suala hilo ni jambo lililoongeza chachu kwa wanadiaspora kutupia jicho zaidi hapa nyumbani wakiahidi kufanya kila wawezalo kuongeza kasi ya uwekezaji hasa katika sekta ya utalii na viwanda.

Washiriki wengi walisema kwamba kongamano la mwaka huu lililofanyika hapa Zanzibar limekuwa na mafanikio chanya wakiakisi kauli mbiu isemayo “Bridging Tanzania Tourism and Investment: A new Outlook” MTU KWAO NDIONGAO ikiwa na lengo la kusisitiza kuunganishwa kwa sekta ya Utalii na Uwekezaji ili kwenda pamoja na kasi ya maendeleo ya Serikali.

Kongamano hili kwa mara ya kwanza linafanyika Zanzibar na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa, lilitanguliwa na Makongamano mawili yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam ambayo nayo pia yamechangia kwa kiasi kikubwa kufikiwa kwa mafanikio makubwa katika kongamano la mwaka huu hapa Zanzibar.

Waziri Gavu alisema kwamba nchi nyingi duniani zinazoshirikiana na diaspora zimefanikiwa kuleta mabadiliko ya kiuchumi kwa vile mchango wao katika sekta uchumi ni mkubwa ikilinganishwa na nchi wahisani.

Kimsingi nakubaliana nae Waziri Issa Gavu kwa sababu kuu mbili;mosi hatutaweza kufikia katika uchumi endelevu ikiwa hakuna fikra mpya, mawazo mapya,pili upya wa mawazo hayo ni lazima uendane na ubunifu wa sera na mipango kama hiyo ya diaspora.

Ushiriki wa Diaspora una faida nyingi hasa katika kuvutia uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje(Foreign Direct Investment-FDI) ambapo FDI ina faida nyingi katika kukuza uchumi wa nchi,kukuza ajira hasa kwa vijana na wanawake, kuongeza fedha za kigeni na kuimarika kwa biashara, usafiri na usafirishaji.

Juhudi zinaochukuliwa na Serikali katika kukuza uchumi, katika kukuza demokrasia na utawala bora ni sehemu ya mikakati ya kuvutia Wawekezaji wenye tija kutoka nje kama uwekezaji wa makampuni makubwa ya nje.

Kama inavyoeleweka Uwekezaji wa makampuni ya nje ni muhimu katika uchumi wa nchi na hususan uchumi wa kileo chini ya biashara huru. Uwekezaji huo unachangia ukuaji wa uchumi wa nchi husika.

Mataifa ya Dunia ya tatu kama Tanzania zinatilia mkazo katika uwekezaji huo wa FDI,pamoja na biashara ya kimataifa ambazo ni chanzo muhimu cha Maendeleo.

Kwa kutambua wajibu huo, Waziri Issa Gavu aliwaleza Wanadiaspora fursa nyingine mpya za miradi ya kiuchumi kama ujenzi, masoko kwa ajili ya biashara mbalimbali, utalii pamoja na uwekezaji katika sekta ya viwanda kwa lengo la kuunga mkono sera ya serikali ya awamu ya tano katika adhima yake ya kujenga Tanzania ya viwanda.

Jambo moja ambalo kwa sasa linaonekana kupenya katika mawazo ya waliowengi ni juu ya namna ya kuwashirikisha Watanzania waishio nje ya nchi katika kuchangia maendeleo ya nchi hii.

Katika hili, nataka kukumbuka maneno ya Mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel mwaka 1979 Agnes Gonxha Bojaxhiu maarufu Mama Teresa alisema " We have not come into the world to be numbered, we have been created for a purpose,for great things to love and be loved" Kwa tafsiri yangu ni kwamba hatukuja duniani kujaza hesa.

Dunia yetu