Untitled Document
home | tume | utangazaaji | znz

Mtoto wa Reagan aomba radhi kwa matamko ya kibaguzi

Rais Richard Nixon akiwa na Gavana Ronald Reagan, kulia, San Diego, California Aug. 16, 1968.

Mtoto wa kike wa rais wa zamani wa Marekani Ronald Reagan ameomba msamaha kwa kauli ya kibaguzi aliyoitoa baba yake.
Reagan alitotoa kauli hiyo mwaka 1971 katika mazungumzo ya simu.
Patti Davis amesema katika maoni yake yaliyochapishwa Alhamisi katika gazeti la Washington Post “ alikuwa hakutarajia kusikia baba yake akitumia neno “nyani” kuwaelezea wajumbe Waafrika waliokuwa wanawakilisha Umoja wa Mataifa ambao walimkasirisha kwa sababu ya kupiga kura.
Wajumbe wa Tanzania walipiga kura mwaka 1971 kulikopelekea UN kuitambua Jamhuri ya Watu wa China badala ya Taiwan.
Katika mazungumzo ya simu baina ya Reagan na rais Nixon, wakati huo Reagan akiwa Gavana wa California alisikika akisema “kuwaona nyani wale kutoka nchi za afrika – (tusi) hata bado hawawezi kuvaa viatu."
Sauti hiyo iliyokuwa haijawahi kutolewa imeibuliwa wiki kadhaa baada ya Rais Donald Trump kutumia lugha ya kibaguzi kuwashambulia wanawake wanne wa chama cha Demokrat wenye asili za mchanganyiko, akikusudia wao siyo Wamarekani halisi na kupendekeza “warejee makwao na kusaidia kutatua maeneo yao wanakotokea yaliyokuwa yameghubikwa na uhalifu
Tim Naftali, aliyekuwa anasimamia maktaba ya rais Richard Nixon na Makumbusho kuanzia 2007 hadi 2011, ameandika kuwa Reagan – ambaye baadae alikuja kuwa Rais wa 40 wa Marekani – alimpigia simu Nixon Octoba 1971, siku moja baada ya Umoja wa Mataifa kupiga kura kuitambua Jamhuri ya Watu wa China.
Katika mazungumzo yake hayo, anasema, Reagan alisikika kwa namna fulani akieleza jinsi ujumbe wa Tanzania ulivyoanza kucheza ngoma katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa wakati kura ya kuruhusu ujumbe kutoka Beijing kuingia uanachama badala ya Taiwan..

Dunia yetu