Untitled Document
home | tume | utangazaaji | znz

Tahadhari juu ya COVID19 yatolewa Zanzibar

Msemaji wa Hospitali ya Rufaa Mnazi mmoja Zanzibar Hassan Makame Mcha (wakatikati) akizungumza na wandishi wa Habari kuhusu kuchukua tahadhari ya maradhi ya Covid 19 na magonjwa mengine hafla iliyofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Hospitali ya Mnazimmoja Mjini Zanzibar.

Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Zanzibar imetoa tahadhari ya kujikinga na maradhi ya Covid 19 yaliyoingia nchini kwa kufuata miongozo inayotolewa na watalamu wa afya.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari huko katika Hospitali ya Rufaa Mnazi Mmoja Msemaji Mkuu wa Hospitali ya hiyo Hassan Makame Mcha amesema wananchi wachukuwe tahadhari za kujikinga ya ugonjwa huo kwa kufuata utaratibu za afya zilizowekwa.

Amesema ugonjwa huo ni wimbi lw tatu ambalo tayari umeshaingia nchini hivyo ni vyema jamii ikafuata miongozo inayotolewa na wataalamu kwa kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima , kuosha mikono kwa maji ya mtiririko pamoja na kuzingatia uvaaji wa barakoa wakati wanapokwenda kuwakagua wagonjwa au kupata huduma.

Msemaji huyo alifahamisha kuwa wananchi wanaotoa huduma kwa wagonjwa wasizidi zaidi ya watu wawili pamoja na kukaa katika vitanda vya wagonjwa ili kuepukana na maambukizi ya maradhi.

“Nawaomba wananchi kupunguza kuja watu wengi wakati wa kuwakagua wagonjwa kwa wakati wote na wanaotakiwa kuhudumia ni watu wawili tu”, alieleza Msemaji huyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Huduma za Uuguzi na Ukunga wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Haji Nyonje Pandu amewataka wananchi kutopuuza maagizo yanayolewa na wataalamu ili kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo.

“Wananchi waache tabia ya kuvaa barakoa wanapotaka kuingia ndani lakini wanakwenda kuwahudumia wagonjwa wanazivua barakoa zao hali hiyo itasababisha ongezeko la maradhi hayo”, alisisitiza Mkurugenzi huyo.

Nae Mkurugenzi Huduma za Tiba wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Dr. Abdulrahman Khalfani Said aliwasisitiza wananchi kutokaidi utaratibu uliowekwa wa uingiaji katika Hospitali ya Mnazi Mmoja ili kuweza kuudhibiti ugonjwa huo usienee kwa kasi nchini..

Other Top Story