Untitled Document
home | tume | utangazaaji | znz

MKUU WA MKOA WA MJINI MAGHARIB MHE IDRISSA KITWANA MUSTAFA AONGEA NA VYOMBO VYA HABARI.

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Idrissa Kitwana azungumza na Waandishi wa Habari katika mafunzo ya kushajihisha Amani, Utangamano na Utamaduni wa kupokea maoni mbadala baada ya Uchaguzi Mkuu katika Ukumbi wa Kitengo cha Uzazi shirikishi Kidongo Chekundu Unguja.

MKUU WA MKOA WA MJINI MAGHARIB MHE IDRISSA KITWANA MUSTAFA AMEZITAKA TAASISI ZA SERIKALI KUTOA USHIRIKIANO KWA VYOMBO VYA HABARI KATIKA KUTOA TAARIFA ILI KUIBUA MATATIZO YANAYOIKABILI JAMII NA KUYAPATIA UFUMBUZI.


HAYO AMEYASEMA WAKATI AKIFUNGUA MAFUNZO YA WAANDISHI WA HABARI JUU YA KUSHAJIHISHA MASUALA YA AMANI,UTANGAMANO NA UTAMADUNI WA KUPOKEA MAONI MBADALA BAADA YA UCHAGUZI MKUU HUKO UKUMBI WA KITENGO CHA UZAZI SHIRIKISHI,KIDONGO CHEKUNDU UNGUJA.

ALISEMA KUFICHA TAARIFA NA KUTOELEZA UKWELI KWA JAMII HUPELEKEA KUWEPO UVUMI NA KUJENGA DHANA POTOFU NA KUTOKUWA NA IMANI KWA VIONGOZI WAO.

AIDHA ALISEMA WANANCHI WANAHITAJI KUPATA TAARIFA ZILIZOSAHIHI ZA MATUKIO YANAYOTOKEA SEHEMU MBALI MBALI YA MAENDELEO, KIUCHUMI NA KISIASA KWA LENGO LA KULETA UFANISI NA KUENDELEA KUWA NA AMANI NCHINI.

MKUU WA MKOA HUYO AMEWATAKA WAANDSHI KUFAHAMU MAFANIKIO, MAENDELEO NA UJENZI WA AMANI YA TAIFA LOLOTE DUNIANI YANAHITAJI ZAIDI UTOLEWAJI WA TAARIFA KUPITIA VYOMBO VYA HABARI BILA YA KUTOKA NJE YA MAADILI YA KAZI.

HATA HIVYO AMEWATAKA WATENDAJI WA VYOMBO HIVYO KUTOCHOKA KUIBUA VIKWAZO VINAVYOWAKABILI WANANCHI NA KUVIFANYIA KAZI PAMOJA NA KUYASEMEA YANAYOTEKELEZWA NA SERIKALI ILI WANANCHI KUYAFAHAMU.

AKIWASILISHA MADA KATIKA MAFUNZO HAYO MWANDISHI MWANDAMIZI ALI SULTAN ALISISITIZA WAANDISHI KUACHA USHABIKI WA MAMBO YASIYO NA FAIDA KWA JAMII PAMOJA NA KUVILINDA VYANZO VYAO VYA HABARI ILI KUEPUKA KUVUNJA AMANI KATIKA FANI HIYO.

MAFUNZO HAYO YA SIKU MBILI YAMEANDALIWA NA KLABU YA WAANDISHI WA HABARI ZANZIBAR ZPC KWA UFADHILI WA INTERNEWS..

Other Top Story