Untitled Document
home | tume | utangazaaji | znzPIZZA YA NYAMA

PIZZA YA NYAMA

MAHITAJI

°Unga wa ngano 1/2
°Amila 1/2 kijiko cha chai
°Nyama yang'ombe au kuku 1/2
°Sukari vijiko 1 1/2 cha mchuzi
°Chumvi kiasi
°Nyanya maji 1 kubwa
°Kitunguu 1 kikubwa
°Jibini kiasi
°Olive oil vijiko 2 vya mchuzi
°Maggie 1
°Pilipili manga 1/2 kijiko cha chai
°Karoti 1
°Hoho 1
°Curry 1/2 kijiko cha chai
°Sosi ya nyanyaJINSI YA KUPIKA
Kwanza, andaa nyama yako ambayo ni steki kata vipande vidogo vidogo kisha tia katika bakuli au sahani,tia maggie,pilipili manga ya unga,chumvi, curry changanya vizuri kisha tia katika friji viungo vikolee.

Chukua bakuli kubwa weka unga wangano,amila,sukari na chumvi kisha changanya kwa pamoja,mimina maji kiasi na ukande una wako hadi uwe laini kisha weka pembeni uumuke kwa dakika kadhaa.

Katakata kitunguu maji,hoho,karoti na nyanya hakikisha unavikata saizi moja, kwa ngua jibini au isage upate unga wake.

Tazama kama ungawako umeumuka kata kidonge kiasi na usukume round kama chapati,inatakiwa chapati unayo isukuma iwe nyepesi ambapo piza yako itakuwa laini itapokuwa tayari,lakini ukifanya chapati nzito piza itakua ngumu maana ukitia katika oven itaumuka pia.

Baada ya hatua hiyo,chukua nyama yako katika friji,chukua trey ya bati ambayo ni pana paka pafuta ya olive kwa chini kisha nyanyua ile chapati na kuikalisha pale, chukua tena olive paka juu ya chapati,kisha chukua souce ya nyanya paka kwa juu katika chapati yote.

Kisha chukua nyama yako weka kwa juu ukitumia staili ya kusambaza utafanya hivyo pia kwa karoti,hoho na nyanya freshi,na mwisho utamalizia unga wa jibini na olive oil kidogo ili kuisaidia kua laini pia.

Baada ya hapo nyanyua trey yako na itie katika oveni acha kwa dakika 30-35-40 piza yako itakuwa tayari kwa kuliwa na haina muda maalum wa kula wala kupika,pia utafurahia upishi wako..

Misosi