Untitled Document
home | tume | utangazaaji | znzUPISHI WA VITUMBUA

UPISHI WA VITUMBUA

Vitumbua ni aina ya vitafunwa vya chai ambavyo hutengenezwa kwa kutumia unga wa mchele.

Kiasili vitumbua ni chakula ambacho hupendelewa sana na watu wa pwani.

Na mara nyingi wamekuwa wakipika kwa kuchanganya na nazi ili kuvifanya view na ladha nzuri zaidi

Mahitaji:

Unga wa mchele ½ kg
Sukari vijiko 4 vya mezani
Tui bubu la nazi
Mafuta ya kupikia
Unga wa hiliki ½ kijiko cha chai
Hamira kijiko 1 cha chai
Chuma cha vitumbua

Maandalizi:

Chukua unga wa mchele na weka kwenye bakuli au sufuria ya kilo moja.

Weka hamira kisha weka sukari kisha miminia tui katika mchanganyiko wako.

Weka hiliki koroga hadi view uji mzito.

Acha uji huo kwa muda wa saa moja hadi uumuke, mara nyingi kuumuka kunategemea na hali ya hewa.

Baada ya hapo weka mafuta kijiko kimoja cha chakula kila kishimo acha yapa..

Misosi